
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema inashirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuchunguza magari 103 yaliyokwama Bandari ya Dar es Salaam kwa kipindi kirefu bila wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
Jumapili, Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo na kubaini kuwapo kwa magari 103 ambayo yameagizwa kwa majina ya taasisi za serikali ikiwamo Ofisi ya Rais, huku akiagiza kufanywa uchunguzi ili kubaini wote walioshiriki katika uingizaji wake.
Kati ya magari hayo, 50 ni ya kubeba wagonjwa (ambulance) yaliyokwama tangu Juni 29, 2015 na magari 53 ya Jeshi la Polisi ambayo yamekwama tangu Juni mwaka huu.
Rais Magufuli alitoa siku saba kwa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Jeshi la Polisi kumpa taarifa kuhusu sababu za magari hayo kukwama bandarini hapo kwa muda mrefu kinyume cha sheria.
Vilevile alimuagiza Mkurugenzi wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola kufanya uchunguzi kwa magari hayo ili kuwabaini wote walioshiriki katika kuingizwa kwake.
Akizungumza na Nipashe jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Takukuru Makao Makuu, Mussa Misalaba, alisema taasisi hiyo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama imeanza uchunguzi huo.
“Tunaendelea vizuri na uchunguzi, tunaendelea kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha linapatikana jibu la kueleweka na ripoti yake ikabidhiwe kwa Rais,” alisema.
Awali, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo, alisema wamepokea maagizo ya Rais Magufuli na wanaendelea kuyafanyia kazi na watahakikisha wanapeleka ripoti ndani ya siku saba kama ilivyoagizwa.
“Rais ametupa maagizo na sisi tumeyapokea na tunayafanyia kazi na tutakapokamilisha, tutampelekea ripoti. Kwa sasa hivi hatuwezi kuzungumza chochote,” alisema.
Post A Comment: