Spika wa Bunge, Job Ndugai ametangaza kuwa jimbo la Singida Kaskazini lililokuwa likishilikiwa na Lazaro Nyalandu liko wazi baada ya mbunge huyo kufutwa uanachama na CCM.


Taarifa iliyotolewa jana Ijumaa na Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa Spika Ndugai amemuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(NEC), Jaji Semistocles Kaijage kumfahamisha kuwa jimbo hilo liko wazi.

Barua hiyo imeandikwa na Spika kwa mujibu wa kifungu 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi 2015 kinachoeleza kwamba, pale ambapo mbunge atajiuzulu, atakufa au sababu nyingine yeyote tofauti na zilizoainishwa katika kifungu cha 113, Spika atamjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kutangaza kwenye Gazeti la Serikali kwamba kiti hicho cha ubunge kiko wazi.

β€œKufuatia barua hiyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaweza kuendelea na mchakato wa kumpata mbunge wa kujaza nafasi hiyo iliyo wazi,” imeeleza taarifa hiyo
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: