KOCHA wa Simba, Joseph Omog, amewataka wachezaji wake kuongeza umakini kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya wenyeji Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine.


Akizungumza na gazeti la Nipashe, Omog, alisema kuwa umakini mdogo hasa kwa safu yake ya ulinzi ilipelekea timu hiyo kutoka sare ya bao 1-1 na Yanga hivyo amewataka wachezaji wake kuwa makini hasa wanapokuwa wanaongoza mchezo.

β€œKama benchi la ufundi kazi yetu tumeifanya, imebaki kazi ya wachezaji uwanjani, lakini tunataka kuona tunapata ushindi, tunapaswa kuwa makini kwa kila dakika uwanjani,” alisema Omog.

Alisema kuwa anaimani kubwa na ushindi kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

β€œMatokeo ya nyuma yamepita sasa tunaangalia mbele, ligi ni ngumu lakini lazima tupambane ili kupata ushindi,” alisema Omog.

Baada ya mchezo wa leo, Simba inayodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa itarejea Dar es Salaam kabla ya kurejea tena Mbeya Novemba 16 kucheza na Tanzania Prisons.

Simba inaongoza kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 16 sawa na Yanga Azam na Mtibwa lakini yenyewe ikiwa na uwiano mzuri wa magoli.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: