KAMA kuna watu wanambeza Laudit Mavugo, basi imekula kwao, kwani straika huyo Mrundi kwa tizi alilokuwa akilipiga kwenye mazoezini ya timu hiyo kujiandaa na mchezo wao wa Jumapili, linaonyesha wazi amerudi kwenye fomu.


Simba inaifuata Mbeya City leo Ijumaa kwa ndege, ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza pointi mbili muhimu mbele ya watani zao Yanga Jumamosi iliyopita, lakini jinsi Mavugo alivyojinoa ni kama ametuma salamu Mbeya.

Simba ilikuwa ikifanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini chini ya makocha Joseph Omog na msaidizi wake Masudi Djuma.

Tangu Jumatatu wiki hii Simba ilipoanza tizi kujiandaa na pambano lao la Mbeya City, mwandishi aliweka kambi na kushuhudia vinara hao wa Ligi Kuu Bara wakipiga mazoezi ya kufa mtu.

Hata hivyo katika mazoezi hayo imethibitika kuwa, straika Laudit Mavugo anarudi baada ya kuyumba tangu atue Msimbazi akitokea Vital' O ya Burundi.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: