
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ni miongoni wa wahitimu waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Uchumi katika masuala ya fedha za kigeni katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Katika mahafali yaliyofanyika jana Jumamosi Novemba 18,2017 wahitimu 79 akiwemo Mwigulu wametunukiwa shahada hiyo katika fani mbalimbali.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais mstaafu Jakaya Kikwete ndiye aliyewatunuku shahada wahitimu hao.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala amesema wahitimu waliotunukiwa jana ni wa awamu ya kwanza.
Amesema kwa kuzingatia uwiano wa jinsi kwa wahitimu wa mwaka huu, asilimia 30 ni wanawake na asilimia 70 ni wanaume.
“Tunawapongeza wahitimu kwa kutimiza vigezo stahiki vya kutunukiwa digrii katika fani na ngazi mbalimbali,” amesema Profesa Mukandala.
Amesema anaamini wamewaandaa vya kutosha kwa ajili ya kujumuika na jamii ya Watanzania katika kutafuta maendeleo.
Post A Comment: