
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MCHUANO mkali wa kuwania nafasi za udiwani kwenye kata 43, unatarajiwa kuwa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokana na vyama hivyo kusimamisha idadi karibu sawa ya wagombea.
Uchaguzi huo unatarajia kufanyika Novemba 26, mwaka huu, na kwa mujibu wa taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), CCM imepitisha wagombea 43 kwenye kata 43, huku Chadema ikiwa na wagombea 42 kwenye kata 43.
NEC ilitaja idadi ya wagombea wa vyama vingine viliowapitisha kuwania nafasi za udiwani kwenye kata hizo kuwa ni ACT-Wazalendo wagombea 18, ADA-Tadea mgombea mmoja, ADC wagombea wanne.
Vingine ni NCCR-Mgeuzi wagombea sita, NRA wagombea wawili, SAU wagombea wawili, TLP mgombea mmoja, UDP wagombea wawili, Chauma mgombea mmoja, CUF wagombea 30, na DP wagombea watatu.
Hadi iku ya mwisho ya uteuzi, kwa mujibu wa NEC, wanachama 22 sawa na asilimia 12.4 ya waliochukua fomu hawakuteuliwa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo kutorudisha fomu, kurudisha fomu nje ya muda uliotakiwa kisheria na fomu kutojazwa ipasavyo.
βWanachama 155 sawa na asilimia 87.6 ya waliochukua fomu za uteuzi walizirejesha na kuteuliwa kugombea. Wanachama 145 sawa na asilimia 93.6 ni wanaume na wagombea 10 sawa na asilimia 6.4 ni wanawake,β ilieleza taarifa hiyo.
Aidha, NEC ilisema wagombea 30 sawa na asilimia 19.4 ya walioteuliwa waliwekewa pingamizi na wagombea wenzao na Msajili wa Vyama vya Siasa kutokana na sababu mbalimbali.
βKwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi kampeni za uchaguzi tayari zimeanza na zitaendelea hadi Novemba 25, mwaka huu, siku moja kabla ya siku ya uchaguzi,β ilisema NEC.
Aidha, NEC ilivikumbusha vyama vya siasa na wagombea kuzingatia maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015 wakati wote wa kampeni na siku ya uchaguzi.
Post A Comment: