Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka 10 jela mfanyabiashara, Gairo Mtozoma (43), baada ya kupatikana   na hatia  kwenye shtaka la kupatikana na silaha pamoja na risasi.


Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa jana Novemba 28 ametoa hukumu hiyo baada ya upande wa mashtaka kudhibitisha kesi pasipo kuacha shaka.

Ni baada ya kupitia ushahidi uliotolewa   na mashahidi watano na utetezi uliotolewa na mshtakiwa mwenyewe.

Mshtakiwa, Mtozoma ambaye ni mkazi wa Magomeni Kagera alikuwa akikabiliwa na kesi ya kupatikana  na silaha ambayo atatumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Na katika shtaka la kupatikana na risasi pia atatumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Wakili wa Serikali,Nassoro Katuga kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo ameomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo. 

Kwa mujibu wa kesi hiyo, mshtakiwa huyo Mtozoma anadaiwa  kuwa Agosti 11,2016 katika eneo la Magomeni Kagera wilaya ya Kinondoni alikutwa akiwa na bastola moja aina ya Browing yenye kumbukumbu  namba 90002 iliyosajiliwa kwa namba TZCAR-A222683 bila ya kuwa na leseni.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Agosti 11,2016 katika eneo hilo la  Magomeni Kagera wilaya ya Kinondoni alikutwa akiwa na risasi 6 bila ya kuwa na leseni.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: