Katika kuhakikisha inafanya vizuri katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa  Simba umemlata mshambuliaji Mnigeria Mussalawal Ibrahim kwa ajili ya majaribio.


Mshambuliaji huyo amefanya mazoezi ya asubuhi na kikosi cha Simba Visiwani Zanzibar kinachojiandaa na mechi dhidi ya Yanga.

Akizungumza tovuti ya Mwanaspoti.co.tz, mshambuliaji  Ibrahim alisema amekuja Tanzania kufanya majaribio na anaimani makocha watamuelewa na ataweza kusajiliwa na timu hiyo.

"Nimetoka kwetu Nigeria kama mchezaji huru na natambua Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wenye uwezo na nimewaona, lakini kwa nilivyoaanza mazoezi mpaka leo, imani yangu nitakubalika," alisema Mnigeria huyo.

"Nitajitahidi kufanya mazoezi ambayo naelekezwa kwa umakini zaidi ili dirisha dogo la usajili likifika jina langu liweze kupita na kusajiliwa na Simba na naimani kama nitapata nafasi hiyo nitatumia uwezo wangu kuisaidia Simba," alisema.

Dirisha Dogo la usajili Tanzania litafungukia Novemba 15, mwaka huu ikiwa ni mechi ya tisa tu tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara Agosti mwaka huu.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: