
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
KASI ya maambukizi ya virusi vya homa ya ini (Hepatitis B) nchini ni kubwa ikilinganishwa na maambukizi ya virusi Vya Ukimwi (VVU), imebainika.
Hali hiyo inatokana na ongezeko la watu wanaokumbwa na ugonjwa na wataalam wamebainisha kuwa ndani ya miezi sita, watu 950 wamegundulika kuwa na virusi hivyo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya ini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. John Rwegasha, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu mradi wa homa ya ini walioufanya mwaka jana kati ya MNH na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa (CDC) cha nchini Marekani.
“Hali ya ugonjwa wa homa ya ini ni mbaya. Tulijiwekea malengo ya kupokea wagonjwa 60, lakini tulikuwa tunapokea wagonjwa 160 mpaka sasa hivi. Kwa muda wa miezi sita tumeshapokea wagonjwa 950 wakati malengo yetu ilikuwa wagonjwa 240,” alisema Dk. Rwegasha.
Dk. Rwegasha alisema tangu waanze mradi huo, mwitikio wa watu kujitokeza ni mkubwa kutokana na ukweli kuwa wengi wao walipata taarifa kupitia vyombo vya habari.
Alisema endapo mwitikio utaendelea kuwa mkubwa, kuna hatari ya idadi ya wagonjwa wa homa ya ini kuongezeka na kufikia 1,800 mwishoni mwa mwaka.
Alisema dawa za ugonjwahuo zipo za kutosha kwa kipindi cha miaka mitano kuhudumia wagonjwa waliobainika kuwa na maambukizi.
Dk. Rwegasha aliongeza kuwa, asilimia 10 ya watu waliogundulika kuwa na ugonjwa huo ndiyo wanaohitaji dawa.
Dk. Tuzo Lyuu wa kutoka kitengo cha dawa MNH, alisema hali ya ugonjwa wa ini nchini inaonekana kuwa kubwa.
Alisema katika utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa nane ya watu wanaojitokeza kuchangia damu wamekutwa wakiwa na maambukizi ya virusi vya homa ya ini.
Alisema katika utafiti walioufanya, waathirika wakubwa ni watu wazima wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea. Alisema vijana na watu wazima wenye umri wa miaka 60 na kuendelea, ndiyo waathirika zaidi hususani wanaume.
Post A Comment: