
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
RAIS John Magufuli, amewaapisha wakuu wa mikoa wapya akiwamo Alexander Mnyeti wa Manyara, makatibu wakuu na manaibu wao, huku akiwaeleza kuwa anachokitarajia kwao ni kuona wanakwenda kuwa watumishi wa wananchi maskini na kuzingatia sheria za nchi.
Hafla ya kuwaapisha viongozi hao ilifanyika Ikulu jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwamo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge, Job Ndugai.
“Mkazingatie sheria na mkawe watumishi wa watu wanyonge. Ninyi ni wawakilishi tu wa Watanzania, mkawe sauti ya wananchi maskini, mkawe wasemaji wao na kila mtakalofanya mkamtangulize Mungu. Nina uhakika mkizingatia haya yote, mtaweza kujibu hoja za Watanzania ambazo ni nyingi,” alisema.
Aidha, Rais Magufuli aliwataka wakuu wa mikoa aliowaapisha jana kwenda kuangalia fursa wanazoweza kuzitumia kukuza uchumi kwenye mikoa yao.
“Na ninyi makatibu wakuu na manaibu mkafanye hivyo hivyo. Mkatatue matatizo haraka kwa kushirikiana na mawaziri na manaibu wenu. Nafahamu kwa mfano tarehe 29 mwezi uliopita niliidhinisha bilioni 147 zikapelekwa Wizara ya Elimu kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wanaostahili,” alisema na kuongeza:
“Najua vyuo vikuu vimeanza kufunguliwa kama siyo wiki hii basi ile inayokuja, sasa nitashangaa sana kama kuna wanafunzi wanaostahili kupata mikopo na wako kwenye orodha ya kupata mikopo wawe hawajapata mikopo… nitashangaa sana kwa sababu najua nimeshaidhinisha Sh. bilioni 147.”
Rais Magufuli alisema ana imani kuwa makatibu wakuu wapya na manaibu wao watatatua haraka changamoto zilizoko kwenye wizara wanazokwenda kuziongoza.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alielezea kutofurahishwa na baadhi ya mambo kwenye Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
“Sifurahishwi kabisa na baadhi ya mambo yanayofanyika pale na ndiyo maana nimeamua kumteua Prof. Adoph Mkenda aliyekuwa Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara kwenda Mambo ya Nje akabadilishe mambo,” alisema
Rais Magufuli alisema baadhi ya watu wameshaigeuza Wizara hiyo kama kijiwe cha kupeleka watu ambao wameshindwa kazi kwenye maeneo yao ili wakapumzike.
“Mtu ameshindwa kazi anapelekwa pale anaambiwa nenda Marekani. Sasa nataka mabalozi kila baada ya muda wawe wanatoa ripoti ya ni wawekezaji wangapi na biashara gani wameleta Tanzania,” alisema Rais Magufuli.
Aidha, alisema kuwa anashangazwa na idadi kubwa ya wafanyakazi kwenye balozi za Tanzania nje ya nchi wakati kazi zinazofanywa zingeweza kufanywa na watu wachache na mambo yakaenda sawa.
“Mfano mdogo tu Brazil ni taifa kubwa lakini wana wafanyakazi wanne tu na wengine wote ni wa muda. Sisi ubalozi wetu hapo Ethiopia unakuta madereva tu wako nane… ndiyo maana nataka Profesa ukaifanyie mabadiliko makubwa,” alisema Rais Magufuli.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, alisema kuna mawaziri wanaokwepa kwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya tano.
Alisema ingawa wamepewa nafasi ya kufanya hivyo kupitia TBC1, wengi wamekuwa wakikwepa na hivyo aliwataka kuzingatia maagizo hayo ili wananchi wajue yanayofanywa na serikali.
WALIOAPISHWA
Katika shughuli hiyo ya kuwaapisha wateule wapya wa nafasi mbalimbali, Rais Magufuli alitangaza mabadiliko ya kituo cha kazi cha Christine Mndeme ambaye sasa, badala ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kama alivyotangazwa awali, amebadilishwa na kwenda Ruvuma huku aliyekuwa mkoani humo, Dk. Binilith Mahenge, akihamishiwa Dodoma. Awali nafasi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma ilikuwa ikishikiliwa na Jordan Rugimbana.
Kwenye uteuzi huo ambao jana wahusika waliapishwa, Rais Magufuli aliwaapandisha vyeo wakuu wa wilaya watatu na kuwateua kuwa wakuu wa mikoa kujaza nafasi za wakuu waliostaafu.
Miongoni mwa waliopandishwa ni Mnyeti ambaye awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru. Hivi karibuni, Mnyeti alikuwa maarufu kwenye vyombo vya habari kutokana na mvutano ulioibuka baina yake na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuhusiana na hatua ya baadhi ya madiwani wa Chadema kutimka chama chao na kujiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mnyeti amekwenda mkoa wa Manyara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Joel Bendera ambaye amestaafu.
Rais Magufuli alimteua pia Joackim Wangabo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya uteuzi huo, Wangabo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na alichukua nafasi ya Kamishna wa Polisi, Zelote Stephen ambaye amestaafu.
Pia Rais Magufuli alimteua Robert Gabriel kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huo Gabriel alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe na baada ya kuapishwa jana, amekwenda kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu.
Naye Adam Malima anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara kuchukua nafasi ya Dk. Charles Mlingwa huku Gelasius Byakanwa akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kuchukua nafasi ya Halima Dendego. Awali Byakanwa alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.
Rais pia alimteua pia aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP mstaafu Ernest Mangu, kuwa balozi.
Kabla ya shughuli ya kuapishwa, taarifa ya Ikulu ilieleza kuwa Mangu pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Aziz Mlima, watapangiwa vituo vya kazi baada ya taratibu kukamilika.
Post A Comment: