
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
WATU 12 wamefariki dunia baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace walilokuwa wamepanda kutoka Mwanza Mjini kwenda Kigongo kuzama katika Ziwa Victoria baada ya kushindwa kusimama katika kituo chake cha mwisho.
Kufuatia ajali hiyo, Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 5:30 asubuhi.
Kamanda Msangi alisema Hiace hiyo ilipata ajali katika eneo la kivuko cha Kigongo kilichopo wilayani Misungwi mkoani humo.
Alisema Hiace hiyo yenye namba T.229 DDW ilikuwa ikiendeshwa na dereva ambaye ni marehemu na jina lake bado kufahamika; ambaye alishindwa kufunga breki na kusababisha gari likiwa na abiria 15 kwenda moja kwa moja ziwani, baada ya kugonga kizuizi cha kuingia kwenye eneo la kivuko.
“Ni kweli ajali imetokea na watu 12 wamekufa wakiwamo watoto watatu," alisema Kamanda Msangi na kueleza zaidi:
"Inasadikiwa gari hilo linalofanya safari zake kutoka Nyegezi kwenda Kigongo Feri lilifeli breki na kusababisha dereva kugonga geti la kivuko hicho na kuelekea ziwani moja kwa moja."
Ajali mbaya zaidi katika Ziwa Victoria ni ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba iliyotokea Mei 21, 1996 na kupoteza maisha ya zaidi ya watu 1,000.
Aidha, Kamanda Msangi alisema majeruhi watatu wapo katika Hospitali ya Bukumbi kwa ajili ya matibabu na miili ya marehemu imeifadhiwa hospitalini hapo kwa ajili ya utambuzi.
Aidha, taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa ilimkariri Magufuli akisema:
“Kwa mshtuko na masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya vifo vya watu 12 waliopoteza maisha baada ya gari la abiria walilokuwa wakisafiria kutumbukia katika ziwa Victoria mkoani Mwanza.
"Nawapa pole sana wote waliopoteza jamaa zao katika ajali hii, nawaomba wawe na moyo wa uvumilivu, ustahimilivu na subira katika kipindi hiki cha majonzi.”
Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi na majeruhi watatu walionusurika katika ajali hiyo wapone haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku, taarifa ya Msigwa ilisema zaidi.
Hiyo ni ajali ya sita katika kivuko hicho ndani ya wiki moja, kwa mujibu wa Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wa mkoa wa Mwanza, Ferdinand Mishamu.
Mishamu alisema ndani ya wiki iliyopita kumetokea ajali tano kutokana na ubovu wa magari, hivyo "ninaomba wakaguzi wa magari wahakikishe hakuna gari lolote ambalo ni bovu litalofanya shughuli za usafirishaji wa abiria katika kivuko hiki."
Post A Comment: