Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemwachia kwa dhamana Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.


Pondà ameachiwa jana Jumamosi jioni baada ya kushikiliwa na Jeshi hilo tangu jana Ijumaa asubuni akituhimiwa kutoa lugha za kichochezi katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumatano iliyopita.

Akizungumza na gazeti la  Mwananchi, Msemaji wa Jumuiya hiyo, Sheikh Rajabu Katimba amesema: "Sheikh Ponda ameachiwa kwa dhamana na atatakiwa kuripoti tena polisi."

Awali, Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa aliliambia Mwananchi kwamba uchunguzi dhidi ya Ponda ulikuwa ukiendelea na kama ungekamilika angepewa dhamana.

"Upelelezi unaendelea na ukikamilika tutaangalia kama atapata dhamana au tutampeleka mahakamani," alisema Mambosasa kabla ya Sheikh Ponda kuachiwa.

Wakili wa Ponda, Profesa Abdallah Safari amesena: "Ni kweli Sheikh Pondà ameachiwa, ni lini atarudi tena sijajua ila sidhani kama watampeleka mahakamani."

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: