Mrisho Gambo amefunguka na kusema Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anapaswa kutambua kuwa yeye kama Mkuu wa mkoa anajishughulisha na matatizo ya watu hivyo kama hatabadili aina ya siasa azifanyazo  basi anapoteza muda wake kwa miaka mitano yote.


Gambo amesema kuwa yeye hana tatizo lolote na Mbunge huyo wa Arusha mjini na kudai kwamba anapaswa kutambua na kubadili aina ya siasa anazofanya kwa kuwa yeye amelenga kutatua matatizo na changamoto za watu wa Arusha Mjini. 

"Msuguano na Mbunge haupo lakini anatakiwa tu asome alama za nyakati kwamba Mkuu wa Mkoa wa sasa amedhamiria kuhangaika na shida za watu kama hatalitambua hilo atapoteza muda wake kwa miaka yake yote mitano" alisema Mrisho Gambo 

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa yeye kama kiongozi kijana anahitaji zaidi kukosolewa kuliko kusifiwa ili aweze kujirekebisha sehemu ambayo ana mapungufu ili aweze kuwa kiongozi madhubuti na mahiri zaidi. 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: