
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, umedai kutaka mabadiliko yafanyike ndani ya Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mpya wa urais.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, amesema Tume ya Uchaguzi haiaminiki na haiwezi kusimamia Uchaguzi utakaokuwa huru na haki kama Mahakama Kuu ilivyoagiza.
Kauli ya Odinga imekuja baada ya kuanza kwa kampeni zao za kwanza jijini Nairobi leo kutokana na uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Juu Ijumaa iliyopita ambapo ilibatilisha matokeo ya ushindi wa Uhuru Kenyatta .
Pamoja na hayo Odinga amekosoa kauli ya Rais Kenyatta ya kuwashtumu Majaji kwa kudai kuwa upinzani hawataki uchaguzi lakini wanataka serikali ya muungano, madai ambayo Odinga amepuuzilia mbali na kusema hawawezi kushirikiana na wezi wa kura.
Kenya inaelekea kwenye Uchaguzi mpya ndani ya siku 60 baada ya Mahakama ya Juu kufuta ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kwa kubaini kuwa, haukuwa huru na haki.
Kenya imekuwa nchi ya kwanza, barani Afrika kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais na kuingia katika vitabu vya historia.
Post A Comment: