
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MEYA wa Ubungo, Boniface Jacob (Chadema), amehojiwa kwa saa tatu na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kwa madai ya kutumia ofisi za umma kufanya vikao vya chama.
Akizungumza baada ya kumaliza kuhojiwa jana jijini Dar es Salaam, Jacob alisema, alitoa utetezi wake kuwa hakufanya kikao isipokuwa alitembelewa na wageni wa chama, lakini kama wanaona anastahili kuwajibishwa wafanye hivyo.
Kadhalika Jacob alisema alitoa ushaidi wa matumizi mabaya ya ofisi za umma, yanayofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
βNimewaeleza Sekretarieti kuwa, pia CCM, kimekuwa kikifanya vikao vyake Ofisi za Ikulu na wamenieleza hakuna aliyewahi kulalamika. Hivyo nimelazimika kuandika barua ya malalamiko juu ya kitendo hicho,β alisema.
Kuitwa na kuhojiwa kwa Jacob na Sekretarieti hiyo kumetokana na kitendo chake cha kumkaribisha ofisini kwake Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani.
Post A Comment: