
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefunguka na kuelezea hali ya Mbunge wa Singida Mashariki na kusema mbunge huyo ameumizwa vibaya na kuwa hali yake toka saa nne za asubuhi jana haikuwa vizuri kutokana na majeraha aliyopata.
Mbowe amesema kuwa Mbunge huyo mpaka sasa bado yupo kwenye chumba cha upasuaji katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya akiendelea kupatiwa matibabu kufuatia kiongozi huyo kupigwa risasi juzi na watu wasiofahamika akiwa mjini Dodoma.
Aidha Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa ambaye naye yupo nchini Kenya amelezea hali ilivyokuwa toka walipofika jana usiku nchini Kenya mpaka dakika za mwisho Mbunge huyo alipoingia kwenye chumba cha upasuaji.
"Mh Tundu Lisu aliwasili usiku majira ya saa saba hapa Nairobi Jomo Kenyatta International Airport na alipokelewa na team ya Madaktari wa Nairobi hospital pale Aairport na matibabu yalianza mara moja kuanzia ndani ya Ambulance hadi hospital.
Aidha alipofika Nairobi hospital alifanyiwa vipimo vyote na baadae saa nne asubuhi aliingizwa chumba cha upasuaji" aliandika Peter Msigwa kwenye ukurasa wake wa facebook.
Mchungaji Msingwa aliendelea kusema kuwa " Tangu jana alipofika alifanyiwa stabilization ili aweze kukabiliana na surgery na zoezi hilo lilifanikiwa vizuri na madaktari wametueleza kuwa hakuna hali yoyote ya hatari na matibabu yake yanaendelea kwa mafanikio hadi sasa majira ya saa 9 alasiri bado hajatoka theatre na madaktari wametueleza kuwa wanaendelea vizuri"
Post A Comment: