Marekani imeeleza kusikitishwa na tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.


β€œTunalaani kitendo hiki cha kipuuzi na cha kutumia nguvu,” imesema taarifa ya Ubalozi wa Marekani nchini iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Ubalozi huo umesema unaungana na Watanzania katika kumtakia kheri Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ili apone haraka.

Lissu jana Alhamisi saa sita usiku alisafirishwa kwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo Nairobi, Kenya.

Awali, alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma baada ya kushambuliwa.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema leo Ijumaa asubuhi kuwa, Lissu alishambuliwa kwa risasi kati ya 28 hadi 32, huku tano zikimpata mwilini.

 Akitoa taarifa ya tukio hilo kwenye kikao cha Bunge, Ndugai amesema risasi mbili zilimpata Lissu kwenye miguu, mbili tumboni na moja kwenye mkono.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: