Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu Omari Mahita amefunguka na kusema katika changamoto kubwa ambayo inalikbali jeshi la polisi Tanzania kwa sasa ni namna ya kudili na wanasiasa na kusema ni kazi kubwa kudili na wanasiasa. 


Mahita alisema hayo juzi  wakati alipokutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kwa sasa IGP Sirro na kusema licha ya changamoto hizo anaamini kuwa jeshi la polisi litasonga kutokana na mikakati ambayo wameweka katika kikao hicho kilichowakutanisha wakuu wa jeshi hilo wastaafu mbalimbali. 

"Kuna changamoto nyingi lakini niwe muwazi tu changamoto ya kwanza ni namna ya kudili na wanasiasa, wanasiasa kudili nao ni kazi kubwa sana lakini nafikiri tutakwenda kutokana na mikakati ambayo tumeweka katika kikao hiki" alisema Mahita 

Omari Mahita amewahi kuwa Mkuu wa jeshi la Polisi nchini Tanzania mnamo mwaka 1996 hadi mwaka 2006 ambapo alistaafu katika nafasi hiyo na kumuachia Saidi A. Mwema ambaye naye alihudumu kwa miaka nane kabla ya kijiti hicho kumuachia Ernest J. Mangu ambaye alihudumu kwa miaka minne kisha baadaye Rais Magufuli alimteua Simon Nyakoro Siro kuwa IGP wa Tanzania. 

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: