Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa (CHADEMA) Tundu Lissu ambaye anapatiwa matibabu nchini Kenya kufuatia kujeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana siku Septemba 9, 2017 amezinduka na kutoa neno kwa Mwenyekiti wa CHADEMA.


Katika ujumbe amboa umewekwa na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa unasema kuwa kiongozi huyo alipopata fahamu aliweza kutoa maneno machache akimtaka Mwenyekiti kuendeleza mapambano.

Tundu Lissu kwa sasa amelazwa nchini Kenya akipatiwa matibabu jijini Nairobi kufuatia kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma siku ya Alhamis saa saba na nusu mchana. 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: