Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuchangia damu katika hospitali zote nchini kwa ajili ya kuienzi damu ya Mwanasheria Mkuu wa chama hicho  Tundu Lissu iliyomwagika jana kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.


Akizungumza na wanahabari jana katika makao makuu ya chama hicho, Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Vicent Mashinji amewaomba wafuasi wa chama hicho waliopo nchini Tanzania kuhakikisha kuanzia leo wanaenda kujitolea damu ili kuwasaidi wagonjwa wenye uhitaji wa damu.

Dkt. Mashinji amesema kuwa, kutokana na  damu ya Lissu imemwagika kabla ya wakati wake ni vyema wanachama nao wakaungana na kwa pamoja kutoa msaada huo ikiwa kama ishara ya kulikomboa taifa la Tanzania.

"Damu ya Lissu imemwagika nyingi sana, lakini watu waliofanya tukio hilo hawajatutisha bali wametuimarisha. Lissu amemwaga damu yake kabla ya muda, Makamanda wote twendeni hospitali zote nchi nzima kuchangia wagonjwa damu. Damu tutakazochangia ni ishara ya kulikomboa taifa letu" Dkt. Mashinji.

Ameongeza kwamba "Nategemea kuanzia leo nitaanza kupata taarifa kutoka mahali mbalimbali nchini Tanzania mkijitolea damu ili kuisaidia benki zetu za damu na wagonjwa wote wakapate huduma ya damu kwa urahisi.

Aidha Mashinji amefafanua kuwa Lissu kupelekwa Jijini Nairobi siyo kwamba hawawamini madaktari wa nyumbani, bali wamehitaji kiongozi huyo aweze kupona haraka akiwa katika mazingira yaliyotulia na yatakayomfanya apumzike kwa amani bila kuweweseka kutokana na tukio lililomtokea Pamoja na hayo Dkt. Mashinji ameweka wazi kwamba matibabu ya kiongozi huyo yatagharamiwa na chama kwa kuwa hawajafuata utaratibu wa bunge unavyohitaji.

"Suala la matibabu ya Mh. Lissu Chama tutagharamia na hatuna wasiwasi katika hilo. Wanachama pamoja na marafiki zetu wapo pamoja nasi na tumeshaanza kupokea michango lakini kama kuna watu wanahitaji kutuchangia kufanikisha matibabu ya Tundu Lissu watu wanaweza kutumia Akaunti Inaitwa CHADEMA M4C Bank ya CRDB tawi la Mbezi 01J0180100600 Tuwashukuru wote na salamu za pole tumezipokea"  Dkt. Mashinji.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: