NI kama muujiza! Licha ya kujeruhiwa vibaya kwa risasi tano zinazodaiwa kumpiga kati ya zaidi ya 20 zinazotajwa kufyatuliwa kwake, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Rais wa Chama cha Wanasheria (TLS), anaendelea kuimarika afya yake.


Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), anaendelea na matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi, Kenya ambako alipelekwa kwa ndege ya kukodi baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana wakati akiwa ndani ya gari nje ya nyumbani kwake, Area D, Dodoma baada ya kutoka bungeni.

Inaelezwa kuwa risasi zaidi ya 20 zilipigwa kwa nia ya kumuondolea uhai wake na tano kati ya hizo ndizo zilizompata.

Akizungumza na gazeti la Nipashe jana, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Abdallah Safari, alisema afya ya Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, inaimarika huku akiendelea na matibabu mjini humo.

Alisema Lissu alionyesha kujitambua na kupata fahamu asubuhi ya juzi, baada ya kufikishwa usiku wa manane nchini Kenya.

β€œTaarifa kutoka huko (Nairobi) zinaeleza afya yake kuimarika, ndiyo taarifa za hadi sasa (ikiwa saa 11 jioni jana),” alisema Profesa Safari.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, juzi alitoa taarifa kwa chama chake huku akiwataka kuwa na subira na kumwombea Lissu arejee katika hali yake ya awali, huku akisema fahamu zimerejea na kuanza kutambua.

Lissu alipigwa risasi tano na watu wasiojulikana juzi mchana wakati akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma akitokea bungeni.

Watu hao wasiojulikana, walidaiwa kutumia gari jeupe aina ya Nissan Patrol, walimshambulia Lissu akiwa ndani ya gari lake, Toyota Land Cruiser, nje nyumbani kwake mjini Dodoma.

Baada ya kujeruhiwa, Lissu alipelekwa katika hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Dodoma na kuanza kuhudimiwa na timu ya madaktari bingwa kabla ya kupelekwa Kenya kwa matibabu zaidi.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: