
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
SHAHIDI wa tatu katika kesi ya kujihusisha na biashara pamoja na kutumia dawa za kulevya, mkemia Domician Dominic (42), amedai mahakamani kwamba alipima mkojo wa mshtakiwa Yusufally Manji mara mbili.
Dominic alisema alipopima sampuli ya mkojo wa mfanyabiashara huyo kwa mara ya kwanza alikuta una chembechembe za dawa zinazotumika kutuliza maumivu makali na za usingizi.
Kadhalika, alidai kuwa vipimo vya awamu ya pili vilionyesha chembechembe za dawa zinazotokana na dawa za kulevya aina ya heroin.
Dominic alitoa madai hayo jana wakati akitoa ushahidi wa Jamhuri dhidi ya Manji anayekabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na biashara pamoja na kutumia dawa za kulevya.
Ushahidi huo ulisikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Cyprian Mkeha, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitals, shahidi huyo wa Jamhuri alidai kuwa alifanya vipimo hivyo baada ya kupokea sampuli ya mkojo wa mshtakiwa aliyefikishwa ofisini kwake akiwa chini ya ulinzi wa Koplo Sospeter.
Alidai kuwa alipoipima sampuli hiyo kwa awamu ya kwanza alibaini kuwapo kwa kundi la dawa za 'Benzodiezepines',
chembechembe ya dawa mbalimbali zinazotumiwa na watu wenye maumivu makali na zinazosababisha usingizi ambazo zinatolewa kwa maelekezo maalumu ya madaktari.
Alidai kuwa katika awamu ya pili ya vipimo vya sampuli hiyo, alibaini 'Metabolities', chembechembe za dawa zenye heroin ambazo zina matumizi sawa na zile za awamu ya kwanza.
Alidai zaidi kuwa baada ya majibu ya vipimo vya sampuli hiyo, aliandaa ripoti na kuikabidhi kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Kutokana na ushahidi huo, Wakili wa utetezi, Hudson Ndusyepo, alipata nafasi ya kumhoji shahidi kama ifuatavyo:
Ndusyepo: Shahidi, dawa zilizopo kwenye kundi la ‘Benzodiezepines’ zinaweza kutumika kama dawa ya maumivu?
Shahidi: Zinaweza kutumika kama dawa za maumivu.
Ndusyepo: Je, zinatolewa na madaktari na zinaweza kumsababishia usingizi mtu?
Shahidi: Kweli, zinaweza.
Ndusyepo: Je, shahidi wakati wa kwenda kutoa sampuli ya mkojo uliingia ndani na mshtakiwa au ulikuwa eneo gani?
Shahidi: Siku hiyo mshtakiwa aliingia chooni na Koplo Sospeter kwa sababu alikuwa chini ya ulinzi na mimi nilisubiri nje... walitoka, wakanikabidhi sampuli ya mkojo nikaanza kufanyia vipimo.
Ndusyepo: Je, shahidi unaweza kuiambia mahakama mkojo ulioupima ni wa Manji au wa askari aliyeingia naye chooni?
Shahidi: Mimi nimepima sampuli ya mkojo nilioupokea kutoka kwa askari aliyekuwa na Manji.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa umefunga ushahidi katika kesi hiyo baada ya kuita mashahidi watatu.
Hakimu Mkeha alisema kwa kuwa Jamhuri imefunga kesi dhidi ya mshtakiwa, mahakama yake itatoa uamuzi wa kama mshtakiwa ana kesi ya kujibu au la kesho.
Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa kati ya Februari 6 na 9, mwaka huu eneo la Upanga Sea View, jijini Dar es Salaam, Manji alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.
Manji ambaye pia ni Diwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mbagala, alikana kutumia dawa za kulevya.
Mbali na kesi ya kutumia dawa za kulevya, Manji (41) anakabiliwa na kesi nyingine ya mashtaka ya uhujumu uchumi mahakamni hapo.
Katika kesi hiyo, inadaiwa Manji na wenzake watatu, pamoja na makosa mengine walikutwa isilivyo halali na vitambaa vya sare za Jeshi la Wananchi (JWTZ) vyenye thamani ya Sh. milioni 236.5.
Kosa la uhujumu uchumi halina dhamana kisheria mpaka kwa ruhusa ya Mahakama Kuu, hivyo Manji amekuwa gerezani tangu mapema mwezi uliopita.
Post A Comment: