
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa takribani wiki moja.
Bulaya alikimbizwa Muhimbili kutoka tarime mkoani Mara baada ya kupata tatizo la kupumua baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya kituo cha polisi mjini Tarime. Alikuwa amelazwa wodi namba 18 katika jengo la Sewahaji akipatiwa matibabu.
Mbunge huyo wa Chadema, jana Agosti 28 ameruhusiwa kutoka hospitali na amewashukuru madaktari wa Muhimbili kwa kumpatia matibabu ya kina.
Amesema afya yake imetengemaa lakini amepewa maelekezo kadhaa.
βKwanza nitapumzika kwa siku 10, hivyo ndivyo nilivyoagizwa na nitatakiwa kurudi tena hospitalini kwa ajili ya kuangaliwa afya yangu zaidi. Kwa sasa nitapumzika kabla ya kurudi jimboni kuendelea na shughuli za maendeleo,β amesema Bulaya.
Bulaya aliwekwa rumande Agosti 18 baada ya kukamatwa na polisi akidaiwa kuingia jimbo la Tarime kufanya shughuli za kisiasa kwa kutoa msaada wa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi kwa mwaliko wa mbunge mwenzake Esther Matiko.
Post A Comment: