
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
UAMUZI wa Rais John Magufuli kutaka utekelezaji wa mradi wa uzalishaji umeme wa maji katika Bonde la Mto Rufiji (Stigler’s Gorge) unadaiwa kusababisha pigo kubwa kwa watu waliokuwa wakijiingizia mamilioni ya fedha kila uchao kupitia miradi ya umeme wa dharura.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Nipashe, ukihusisha mahojiano na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya nishati ya umeme, umebaini kuwa kupitia mradi huo wa bonde la Rufiji lililoko mkoani Pwani, taifa litaondokana jumla na ulipaji wa mabilioni ya fedha kugharimia miradi ghali ya umeme wa mafuta na vyanzo vingine visivyokuwa vya maji, hivyo kufuta upenyo wa ‘dili’ mbalimbali zenye kuligharimu taifa.
Jana, akizindua Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya jijini Dar es Salaam (Sabasaba), yanayokutanisha kampuni 55 kutoka Ulaya na zaidi ya 2,500 kutoka Afrika, Rais Magufuli alisisitiza kuwa iwe mvua, jua, mradi wa Stiglers ni lazima uanze, hivyo kuliwezesha taifa kuwa na uwezekano wa kupata umeme wa uhakika unaotazamiwa kufikia kiwango cha Megawati zaidi ya 2,100. Hivi sasa, vyanzo vyote vya umeme nchini huzalisha Megawati 1,400.
Hata hivyo, uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa mradi huo uliokwama kuanza kwa miaka mingi kabla ya ujio wa serikali ya awamu ya tano, unatishia maslahi ya kiuchumi ya baadhi ya watu waliokuwa wakinufaika kila uchao kupitia uzalishaji wa umeme kwa vyanzo vya dharura.
“Miradi ya aina hii huwa haipendwi na baadhi ya watu. Inahatarisha dili za fedha nyingi na ndiyo maana vikwazo huwa haviishi,” mmoja wa wachambuzi aliiambia Nipashe na kuongeza:
“Wengine husingizia masuala ya mazingira, wengine huwatumia watu wanaozungumzia gharama kubwa na sababu nyingine mbalimbali. Uzuri wake ni kwamba JPM (Rais Magufuli) anayajua yote hayo ndiyo maana ameshikilia uzi ule ule kwamba mradi huu ni lazima utekelezwe.
“Hii ni habari njema sana hasa katika kipindi hiki ambacho taifa limepania kujielekeza katika uchumi wa viwanda. Ni kwa sababu umeme wa maji ndiyo wa gharama nafuu kuliko wa vyanzo vingine vyote.”
Kwa mujibu wa ripoti ya utafi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) kuhusiana na maji kama msingi wa chakula na nishati barani Afrika ya mwaka 2008 (www.fao.org), umeme maji umeme wa maji ndiyo wa gharama nafuu kuliko wote, wenye kujali zaidi mazingira na ndiyo maana hutegemewa zaidi na nchi zilizoendelea za Canada, New Zealand, Norway nad Sweden.
MRADI WA STIGLER’S GORGE
Akizungumza jana, Rais Magufuli alisema Serikali yake imedhamiria kuanza mradi wa kuzalisha umeme kwa maji wa Stigler's Gorge ambao unagusa kipande cha mbuga ya Selous ili kuzalisha umeme mwingi wa megawati 2,100.
Alisema licha ya baadhi ya mataifa kupinga mradi huo kwa kile kinachodaiwa kwamba kutakuwapo na athari za mazingira, mradi huo ni lazima utajengwa kwa namna yoyote ile kama serikali yake ilivyopanga.
"Mvua inyeshe, jua liwake, iwe usiku au mchana, Stigler's Gorge lazima ijengwe. Nimeshatoa maelekezo kwa wahusika, tender itatangazwa na mradi utajengwa,” alisema Rais Magufuli.
“Haiwekezani tuzungumze nchi ya viwanda halafu viwanda visiwe na umeme. Na ninawaeleza, hatutasikikiza suala la environmental impact assessment ( tathmini ya athari za kimazingira)," alisema Rais Magufuli, ambaye alifafanua kuwa eneo la mbuga litakaloguswa ni dogo tu kiasi cha asilimia tatu, hivyo hilo haliwezi kuwa kikwazo kwa mradi huo. Mbuga ya Selous ina ukubwa wa kilometa za mraba 45,000 na mradi wa Stigler's una ukubwa wa kilometa za mraba 1,350.
Rais Magufuli alisema mradi huo wa kuzalisha umeme pindi utakapokamilika utawezesha kupatikana kwa umeme wa uhakika utakaotumika katika uzalishaji viwandani.
Alisema serikali haitasikiliza mtu yeyote kuhusu ujenzi wa mradi huo mkubwa.
Aidha, alisema kukamilika kwa mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi wenye uwezo wa kuzalisha umeme megawati 4,000, Tanzania itakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme zaidi ya megawati 5,000, ikiwa ni kwa pamoja na umeme huo wa Stigler's Gorge.
"Kwanza mradi huo ukikamilika ndiyo utapunguza athari za mazingira, samaki wataongezeka, uvuvi utaongezeka, ndege, Kilimo kitapanuka na kuongeza malighafi viwandani, sasa wanaopinga na wapinge," alisema Rais Magufuli.
Alisema Tanzania ina malighafi nyingi za kuzalisha nishati ambazo bado hazitumiwi na wazawa bali na baadhi ya wageni wanaotumia udanganyifu, akizitaja baadhi ya malighafi hizo kuwa ni makaa ya mawe.
Alizitaja nyingine zisizotumika ipasavyo kuwa ni pamoja na umeme wa upepo, madini ya uranium, jotoardhi (geothermal) na mito mikubwa.
Rais Magufuli alisema anachokifanya kwa sasa ni kuhakikisha Watanzania wananufaika na maliasili zilizomo nchini na kwamba wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi wanapaswa kuisaidia serikali katika kuleta maendeleo.
"Nataka kuwahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu salama. Tanzania ipo kwa ajili ya wawekezaji, lakini uwekezaji uwe na manufaa hata kwa Tanzania, huu ni wakati wa kuibadilisha nchi. Tanzania tulichezewa mno, ni lazima tubadilike," alisema Rais Magufuli.
Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, alisema kufanyika kwa maonyesho ya 41 ya biashara kwa mwaka huu kutasaidia nchi kupata fedha za kigeni pamoja na kutangaza bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kama vile asali na bidhaa za ngozi.
WABUNGE WAUNGA MKONO
Mbunge wa Same Mashariki (Chadema), Naghenjwa Kaboyoka, alisema mradi wa Stigler’s Gorge utaokoa fedha ambazo serikali imekuwa ikitumia kugharimia umeme wa mafuta ambao kwingineko huwa ni wa dharura.
Akizungumza na Nipashe, Kaboyoka ambaye pia ni Mbunge wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema nchi inapotaka kwenda kwenye uchumi wa viwanda, umeme wa kutumia dizeli au petroli ni wa gharama kubwa na haufai kiuchumi bali wa kuzalishwa kwa maji.
Alisema umeme wa maji ndio wa gharama nafuu na mradi wa bwawa hilo utatoa umeme mwingi kwa gharama nafuu na hivyo ni lazima kuangalia kuwa hayo mazingira yataharibika kwa kiasi gani kukijengwa umeme na yakahifadhiwa.
Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali, alisema kadri anavyofahamu, haamini kuwa kuna watu walikuwa wakikwamisha kusudi mradi wa Stigler’s Gorge bali inawezekana kuwa tatizo lilikuwa fedha na uthubutu.
“Kitu ninachoweza kusema ni kwamba Naunga mkono mradi huo kwa asilimia 100 kwani hatuwezi kupata maendeleo kama hatuna nishati ya umeme ya uhakika na hatuwezi kuwa na uchumi wa viwanda kama hatuna umeme wa uhakika,” alisema Bobali, lakini akisisitiza kuwa kivutio siyo umeme pekee bali pia malighafi ambazo zitapatikana kwa kuwekeza katika kilimo.
Credit - Nipashe
Post A Comment: