Idadi ya watu waliofariki kwa kuungua kwa moto nchini Ureno imeongezeka na kufikia 62.


 Awali waliripotiwa watu 19, baadaye idadi hiyo iliongezeka na kufikia 25 ambayo mpaka sasa imefikia 62

Kwa mujibu wa maofisa wa serikali nchini humo, wengi walifariki walipokuwa wakiukimbia mji wa Pedrogao Grande, kilomita 50 kama (Maili 30) Kusini mashariki mwa Coimbra, kwa kutumia magari yao.

Maofisa wa Ureno wamesema kuwa, moto huo ulianza katika maeneo ya katikati mwa nchi hiyo na kusababisha vifo hivyo huku watu wengine  wakijeruhiwa  wakiwamo maafisa kadhaa wa zima moto.

Mpaka sasa chanzo kilichosababisha moto huo hakijabainika.

"Hili linaonekana ni janga baya zaidi ambalo tumewahi kushuhudia katika miaka ya hivi karibuni, katika moto wa nyika," amesema Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Antonio Costa.

Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo João Gomes, amewaambia waandishi habari kuwa, watu 16 wameteketea ndani ya magari yao hadi kufa, wakati walipojaribu kukabiliana na moto huo mkubwa.

 “Moto huo ulienea kwa kasi mno katika maeneo manne,” amesema Gomes.

Hispania imetuma ndege mbili  zitakazosaidia kuuzima moto huo.


ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: