Timu ya Soka ya Taifa ya Tanzania ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys leo imefanikiwa kuichapa Angola kwa mabao 2-1, ikiwa ni mechi yao ya pili ya michuano ya AFCON.


Mechi hiyo ya kundi B iliyovuta usikivu wa Watanzania wengi waliokuwa wakifuatilia kupitia vyombo vya habari na kujadilia kupitia mitandao ya kijamii, ilishuhudia timu hizo mbili zikitoka sare ya 1-1 katika kipindi cha kwanza. Goli la Serengeti Boys likifungwa na Kelvin Nashon Naftali kwa kichwa sawia katika dakika ya 6, na Angola ikisawazisha katika dakika ya 17 kupitia Da’ Silva.

Kipindi cha pili kilianza kwa nguvu za kila timu kusaka goli la ushindi, hadi dakika ya 69 ambapo Abdul Hamis Suleiman alipokata mzizi wa fitna kwa kutikisa nyavu za Gabon na kuipa Serengeti Boys goli la ushindi.

Kwa matokeo hayo, Serengeti Boys ndio wababe wanaoongoza kundi B kwa kuwa na pointi 4 huku wakisubiri kukutana na Niger wiki ijayo.

Harufu ya Serengeti Boys kutinga katika fainali za Kombe la Dunia zitakazotimua vumbi nchini India inaanza kuzigusa pua za wengi, kilichobaki ni maombi na nguvu ya ziada.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: