Msemaji wa Klabu ya Simba aliyefungiwa na TFF, Haji Manara amefunguka mengine mapya kwa kudai bado hajakubaliana na ubingwa wa ligi kuu Tanzania walioutwaa Yanga SC na kudai kuwa wao (Simba SC) ndiyo mabingwa wa ligi hiyo msimu huu.


Manara amebainisha hayo kupitia mitandao ya kijamii kwa kurusha vijembe kwa wapinzani wao wa jadi na kudai kwamba kama Serengeti Boys waliweza kushinda rufaa yao na kuweza kushiriki michuano ya vijana huko nchini Gabon basi nao watashinda bila shika.

"Wabongo bana kwa 'double standard' hawajambo, Serengeti Boys walikuwa Gabon kwa kushinda rufaa ila Simba hawastahili....Mjiandae kiakili Gongowazi, Simba ndiyo 'champion' msimu huu". Ameandika Manara

Tayari Simba imewasilisha malalamiko yao kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) wakipinga kupokwa pointi 3 na TFF baada ya kupewa na bodi ya ligi kutokana na Kagera Sugar kumtumia mchezaji asiyestahili katika mechi dhidi yao, ambapo Kagera Sugar ilipata ushindi wa mabao 2-1.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: