
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
ALIYEKUWA Straika wa Azam FC, Kipre Herman Tchetche, amesema licha ya kutofuatwa na timu yoyote kutoka Tanzania, lakini yupo tayari kurejea nchini kujiunga na Simba au Yanga kama timu hizo zitahitaji huduma yake.
Kipre ni miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa wakitajwa mara kwa mara katika usajili wa klabu ya Yanga, huku baadhi ya vigogo kupendekeza jina la straika huyo anayekipiga katika klabu ya Al- Nahda Al Buraimi ya Oman.
Yanga imefikia hatua ya kumtaja Kipre baada ya straika wao, Donald Ngoma, kugomea uongozi wa klabu hiyo kuongeza mkataba mwingine, huku ikidaiwa kwamba amepata timu Afrika Kusini.
Kipre alisema, kwamba kwa sasa anasubiri msimu umalizike ambapo wanacheza michuano ya kombe la Majesty, baada ya hapo hajajua ataelekea wapi.
Alisema hadi sasa hakuna kiongozi wa timu yoyote kutoka Tanzania aliyempigia simu kumpa taarifa hizo, lakini kama itatokea yupo tayari kurejea na kucheza soka Tanzania.
“Hizo taarifa za Yanga sijazisikia wala kufuata, kwani bado sijajua hatima yangu hadi hapo nitakapomaliza msimu, suala la dau kwa sasa ni siri yangu kwa timu inayonihitaji,” alisema Kipre.
Post A Comment: