Katika hali ya kuleta matumaini na kuonyesha njia ya mafanikio Rais wa
Sudan Kusini Salva Kiir amelivunja bunge lake na kuunda serikali ya
umoja,katika mapambano ya kuleta makubaliano ya amani ili kumaliza vita
vya wenyewe kwa wenyewe miaka miwili
Thuluthi
moja ya mawaziri wa bunge hilo jipya ni wanachama wa chama cha SPLM-IO
kilichobuniwa na aliyekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar,ambaye alirudi
mjini Juba mapema wiki hii ili kuapishwa kuwa makamu wa kwanza wa rais.
Maelfu ya raia wameuawa na watu milioni 2 wakiwachwa bila makao katika mgogoro huo wa Sudan Kusini ambayo ilipata uhuru wake mwaka 2011.
Aidha mpango huo unaowashirikisha waliokuwa waasi katika serikali ulitangazwa Alhamisi katika runinga ya taifa.
Chanzo BBC

DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: