Serikali inatarajia kununua mipira ya kiume (kondomu) zitakazosambazwa nchi nzima bure, kwa lengo la kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ifikapo 2030.


Taarifa hiyo imetolewa jana Novemba 27,2017 na Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibamaila, wakati wa uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa kondomu.

Amesema kuwa suala kutakuwa na mashine maalumu zitakazofungwa kwenye maeneo ya sehemu za starehe kama baa, nyumba za kulala wageni, migodini na katika kumbi za burudani.

Ameeleza kuwa takwimu zinaonyesha licha ya kuwa na ufahamu wa faida ya kondomu, idadi ya wanaotumia ni chache zaidi.

β€œTakwimu zinaonyesha kwamba 69% ya wanawake na 77% ya wanaume wanafahamu kwamba kondomu inaweza kuzuia VVU, lakini ni 27% tu ya watu wenye wenza zaidi ya mmoja walitumia kondomu walipofanya ngono mara ya mwisho,” amesema.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: