Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amesema hata kama gharama za  matibabu ya Tundu Lissu yakifika Trilioni  moja, watakuwa tayari kuuza figo zao.


Akizungumza jana Novemba 18 katika kata ya Siuyu iliyopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Lema amesema utekelezaji wa  majukumu ya kisiasa ukiwa upinzani wakati huu ni ngumu kutokana na kuwindwa kila uchao.

Amesema  pamoja na ugumu huo hawajarudi nyuma na kisasi cha wasiopenda mabadiliko na wanaochukia kukosolewa   kimedhihirika  kwa vitendo alivyotendewa Lissu.

"Lissu yupo kitandani risasi mwili mzima, gharama za matibabu yake ni kubwa, lakini hata ikifika trilioni moja na tukawa hatuna fedha tutauza figo zetu kuendelea kugharamia matibabu yake" amesema Lema.

Amesema Lissu amekuwa alama ya haki katika taifa kutokana na kuamua kuwa upande wa haki.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: