Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amesema uhakiki wa vyeti ni changamoto aliyokumbana nayo alipokuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na hataweza kuisahau ingawa anashukuru jinsi alivyopata ushirikiano.
Mh. Kairuki amesema hayo leo wakati wa kukabidhi ofisi kwa Waziri mpya wa Utumishi George Mkuchika aliyeteuliwa na kuapishwa mwanzoni mwa wiki hii ambapo amesena kwamba japo kazi hiyo ya changamoto ilichukua muda mrefu hadi kufikia kuwakatisha tamaa watumishi wa umma lakini aliimaliza vizuri.
"Nchi kama vile Afrika Kusini, India na Pakistan walifanya jambo kama hili kwa awamu mpaka nne na bado hawajamaliza, lakini sisi tumelifanya kwa jumla ingawa imechukuwa muda mrefu mpaka watumishi wakaanza kukasirika na haikuwa kazi nyepesi," amesema.
Pamoja na chanmgamoto hiyo Kairuki amesema baadhi ya watendaji alioshirikiana nao hawakuwa waaminifu ambao walipenyeza watu wasiokuwa na sifa jambo ambalo amemtaka Waziri Mkuchika kupambana nao ipasavyo.
Aidha ameongeza kwamba suala la maslahi ya watumishi wa umma lilikuwa changamoto nyingine kwa sababu serikali inatamani kuyaboresha lakini fedha inayokusanywa haikidhi mahitaji.
Mbali na hayo amewatoa shaka watumishi ambao hawajapandishwa madaraja akifafanua kwamba fedha kwa ajili watumishi zaidi ya 163,000 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza suala hilo la maboresho.

Post A Comment: