Rais mstaafu, Jakaya Kikwete amesema amefurahishwa namna Serikali ilivyojidhatiti kukarabati shule kongwe nchini ikiwamo Sekondari ya Kibaha, mkoani Pwani.


Kikwete alisema hayo juzi alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 50 ya kidato cha nne shuleni hapo, huku wanafunzi 116 wakihitimu katika michepuo ya sayansi, kilimo na biashara.

β€œKwa upande wa uhaba wa madarasa nitashirikiana na wadau wengine kuona namna ya kusaidia kutatua changamoto hiyo, kwa hadhi ya shule hii haipendezi kuwa na mrundikano wa wanafunzi darasani,” alisema Kikwete ambaye alisomea shule hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alisema umefika wakati watu waliosoma katika shule hiyo kuangalia namna ya kuweka mipango madhubuti kusaidia kuboresha miundombinu.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha, Profesa Patrick Makungu alisema tangu shule hiyo ilipoanzishwa mwaka 1965, imeendelea kutoa wahitimu wa kidato cha nne na cha sita wengi wao waliendelea na masomo ya elimu ya juu na kurudi kuitumikia Serikali kwa kushika nafasi mbalimbali.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: