Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limekamata magari nane aina ya Nissan Patrol yenye rangi nyeupe na kuyafanyia ukaguzi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusiana na tukio la kusambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu .


Tukio hilo lilitokea Septemba 7 mwaka huu nyumbani kwake Area D Dodoma, wakati mbunge huyo akirejea nyumbani akitoka bungeni.

Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 9 na Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.

"Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa wahalifu walikuwa na silaha ya SMG/SAR kutokana na maganda ya risasi yaliyokutwa eneo," amesema Muroto

Hata hivyo Kamanda Muroto amemtaka dereva wa Lissu, aliyemtaja kwa jina la Adam kujitokeza kituo cha Polisi ili aweze kutoa maelezo yake kuhusiana na tukio la kupigwa risasi kwani yeye ndiye alikuwa naye siku ya tukio.

Pia Kamanda Muroto amemtaka Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Vicent Mashinji kufika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Dodoma au Makao makuu ya upelelezi Dar es salaam ili kutoa ushahidi kuhusu tukio hilo.

Alifafanua kuwa Mashinji katika mkutano wake na waandishi wa habari alidai kuwa anawafahamu watu waliofanya shambulio hilo kwa hivyo amemtaka kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi .
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: