
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MKOA wa Rukwa umezuia usafirishaji wa tani 2,143 za udongo wa kutengeneza sementi kutokana na kile kilichodaiwa kuwa kuna ubabaishaji.
Mkuu wa mkoa huo Zelote Steven, alipiga marufuku kuuza udongo huo unaitwa ‘clinker’ kufuatia ubabaishaji kwenye usafirishaji wa kuyapeleka madini hayo nje, hadi hapo itakapodhihirika kuwa utaratibu unaotumiwa ni sahihi.
Alisimamisha usafirishaji wa madini hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Kasanga wilayani Kalambo baada ya kupata taarifa za siri kuwa madini hayo yanasafirishwa kwenda Kongo kwa kupitia Ziwa Tanganyika.
Usafirishaji wa mawe hayo umekuwa ukifanywa na kampuni ya Mbeya Cement ya jijini hapa tangu Februari mwaka huu na kuiuzia kampuni ya Burundi Cement ya jijini Bujumbura, hadi mkuu wa mkoa alipozuia uuzwaji huo, tayari walikuwa wameshauza tani 4,760 huku tani moja ikiuzwa kwa Dola 128 karibu sawa na Shilingi 300,000.
Wakati Zelote akiendelea na ukaguzi katika bandari hiyo aligundua kuwa kampuni hiyo ya Mbeya Cement ina mzigo wa tani 2,050 za mifuko ya saruji iliyopo bandarini hapo tangu mwezi Novemba mwaka 2016 na alipomuuliza mwakilishi wake, Sabas Sokoni alisema saruji hiyo imekosa wateja.
“Sisi tunajua kwamba bandari hii inapokea sementi na kuuzwa nchi za jirani, haya ni madini, haiwezekani tukadanganya kwamba tunapeleka madini kumbe tunapeleka “malighafi ndiyo raw materials” kutoka Tanzania kwa ajili ya kutengeneza sementi..”
“Kila siku tunazungumza suala la kuongeza thamani ya vitu vyetu ili tuuze bidhaa zilizoboreshwa na sio “raw materilas.” Alionya.
Aliongeza kusema kuwa utaratibu uliopo ni kwamba sementi inazalishwa Tanzania na kuuzwa nje ya nchi na sio kusafirisha udongo wa kuitengenezea na kuhoji kuwa kwanini udongo huo uwe na soko zaidi kuliko sementi?
Wakati mkuu huyo wa mkoa akitoa zuio hilo tayari tani 800 zilikuwa zimo kwenye meli ya MV Tora yenye namba za usajili BY 0064 huku ikiwa na bendera ya Burundi tayari kwa kusafirishwa kwenda nchini humo.
Kwa upande wake Ofisa wa Bandari ya Kasanga, Suleiman Kalugendo, alisema hakuona tatizo katika suala zima la usafirishaji wa madini hayo licha ya kuwa vibali vya usafirishaji wa madini hayo kuwa na mashaka.
Post A Comment: