Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wanachama wa chama hicho kutokata tamaa wakiamini haki walioipata kupitia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 itapatikana hivi karibuni.


Maalim Seif alisema hayo wakati akiwahutubia wanachama wa chama hicho katika mkutano mkuu wa Jimbo la Mtoni Wilaya ya Magharib A Unguja.

Seif alisema katika chama hicho wapo baadhi ya watu wamekuwa wakihisi kile anachokisema ni uongo.

Akizungumzia kuhusiana na kadhia inayoendelea kukikumba chama hicho alisema kwa sasa kila kitu kipo mahakamani na anaamini ndiyo chombo pekee cha kutoa haki kwa mujibu wa sheria.

Pia, Maalim Seif aliwahakikishia wanachama hao kuwa chama hicho kitaendelea kubaki salama licha ya misukosuko inayoendelea hivi sasa.

Awali, akifungua mkutano huo, Makamu Mwenyekiti Mstaafu Juma Duni Haji alisema CUF haipo tayari kuona damu inamwagika.

β€œChama hiki kitaendelea kubaki salama kama walivyokikuta wale wote wenye nia mbaya, watadhalilika na kuonekana na kila mtu kama wenzao,” alisema Haji.     
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: