Pamoja na kwamba simu zimeleta maendeleo makubwa katika teknolojia ya Mawasiliano duniani lakini betri zinazotumika katika simu hizi hasa katika simu aina ya smartphone zimeonekana kuwa na sumu kali inayoweza kudhuru afya ya binadamu.


 Katika tafiti mpya zilizofanyika hivi karibuni imegundulika kuwa zaidi ya gesi 100 zinazoweza kusababisha kifo hutolewa na betri zinazopatikana miongoni mwa mabilioni ya vifaa vinavyotumiwa na raia wengi duniani zikiwemo simu aina ya smartphone na vipatakilishi.

Utafiti huo ulibaini kuwa betri za lithium zinazotumika sana katika simu aina ya smartphone hutoa aina 100 za gesi zenye sumu kali ikiwemo gesi ya kaboni monoksaidi, ambayo inaweza kusababisha kujikuna katika ngozi, macho na pua pamoja na kuathiri mazingira.

Watafiti kutoka Taasisi ya Ulinzi ya NBC nchini Marekani pamoja na Chuo Kikuu cha Tsinghua nchini China wamesema kuwa watu wengi huenda hawajui hatari ya betri kupata moto, kuharibika ama kutumia chaji isiofaa katika vifaa hivyo, jarida la Science Explorer limeripoti.

Katika utafiti huo mpya wataalam walichunguza betri moja ya kuchaji inayojulikana kama Lithium-ion,ambayo huwekwa katika vifaa vinavyotumika kila mwaka na kubaini kuwepo kwa sumu kali katika betri hiyo.

”Siku hizi, Betri za Lithium-ion hukuzwa na serikali nyingi duniani kama kawi inayopatikana kwa haraka ili kuviwasha vifaa vyote ikiwemo magari ya kielektroniki hadi simu,” alisema Jie Sun, Profesa Mkuu katika Taasisi ya Ulinzi ya NBC.

Sun na wenzake waligundua sababu kadhaa ambazo zinaweza kuongeza gesi zenye sumu zinazotolewa ambapo walithibitisha kuwa betri zilizopata chaji zaidi hutoa gesi zaidi za sumu ikilinganishwa na betri ilio na asilimia 50 ya chaji.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: