Mfanyabiashara tajiri Afrika, Aliko Dangote anasubiri idhini ya Benki Kuu ya Nigeria ili anunue kiwanda cha kuunda magari aina ya Peugeot akishirikiana na majimbo mawili.


Kampuni ya Usimamizi wa Mali ya Nigeria (AMCON), iliyoundwa wakati wa kuyumba kwa benki, inakaribia kuuza Kiwanda cha Magari cha Peugeot cha Nigeria (PAN).

“Tumeshakamilisha mchakato wote wa zabuni miezi miwili iliyopita na sasa tunasubiri idhini ya Benki Kuu,” alisema ofisa mtendaji mkuu wa AMCON, Ahmed Kuru alipoongea na Reuters.

PAN, kiwanda cha kuunda magari kilichopo jimbo la Kaduna, kina ubia wa kiufundi na PSA Peugeot Citroen na kikiwa na uwezo wa kuunganisha magari 90,000 kwa mwaka.

Dangote, kwa kushirikiana na majimbo ya Kaduna na Kebbi na Benki ya Viwanda (BOI) waliomba zabuni ya kuwa wamiliki wakubwa wa hisa za PAN mwaka jana kutokana na AMCON kutaka kuuza baadhi ya mali zake ilizozichukua wakati wa matatizo ya taasisi za kifedha.


ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: