Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimemtaka Kaimu Jaji Mkuu, Prof Ibrahim Juma kukemea hadharani shambulizi lililofanyika katika ofisi za mawakili za IMMMA.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen Kijo-Bisimba amesema tangu kutokea mlipuko usiku wa kuamkia Agosti 26, hakuna kiongozi wa Serikali ambaye amejitokeza na kukemea tukio hilo na kitendo hicho kimewatia hofu Mawakili nchini.

Alisema Kaimu Jaji Mkuu anayesimamia mhimili wa Mahakama naye amekaa kimya kama vile hakuna tukio lolote lililotokea.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu kupitia Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Benedict Kitalika, jana limesema watu waliovamia ofisi hizo na kuzilipua walikuwa wamevaa sare zinazofanana na Jeshi la Polisi lakini si askari wake.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: