Wizara ya Fedha na Mipango imeliomba Bunge iliidhinishie Sh11.757trilioni ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote tisa yaliyo chini ya Wizara hiyo.


Maombi hayo yametolewa leo na Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mpango, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizaya hiyo, Bungeni Mjini Dodoma.

 Dk Mpango amesema kuwa kati ya fedha hizo, Sh10.328trilioni  ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh1.429trilioni  ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

 Amefafanua kuwa matumizi ya kawaida yanajumuisha Sh87.996bilioni kwa ajili ya mishahara, Sh778.6bilini kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC) na Sh9.4trilioni ni kwa ajili ya kulipa Deni la Taifa na Huduma nyingine.

 Pia katika fedha za matumizi ya maendeleo, Sh1.382trilioni  ni fedha za ndani na Sh46.1bilioni ni fedha za nje.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: