ads

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, linawashikilia watu watatu wanaodaiwa kuwa majambazi kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha na kupora Shilingi milioni 464 milioni.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema, watu hao walikamatwa Julai 19 mkoani Singida walipokimbilia baada ya kufanya uhalifu na kusema kuwa watu hao walikamatwa na fedha halali za Kitanzania Shilingi milioni 40 na Dola za Marekani 190,000 na silaha aina ya Short gun vilivyoibiwa katika kiwanda kinachojihusisha na biashara ya mabondo ya samaki cha Weish AST Ltd jijini Mwanza .

Aidha Kamanda Msangi amewataja watu hao kuwa ni Seif Waziri, Daud Mwakalinga wote wakazi wa Dodoma waliokamatwa wakiwa mkoani Singida wakiwa wamebaki na Shilingi milioni 2 na Dola za Marekani 20,000 huku Emmanuel Mwakilili aliyekamatwa jijini Mwanza baada ya kutajwa na wenzake.

Kwa mujibu wa Kamanda Msangi amesema tukio hilo la uporaji lilitokea jijini Mwanza Julai 14, mwaka huu ambapo majambazi watano walivamia kiwanda hicho wakiwa na silaha za jadi na kumpiga mlinzi na kitu kizito kichwani na kumpora silaha kisha kuingia ndani na kupora kiasi hicho cha fedha na kutokomea kusikojulikana.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: