ads

Baada ya kumaliza Mkataba wake ndani ya klabu ya Yaanga, Kocha wa Yanga Mzambia George Lwandamina, tetesi kutoka kwenye uongozi wa Yanga umekiri kuwa wanategemea kumpa mkataba mpya kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara.


Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesikika akikiri kuwa ni kweli kocha huyo mkataba wake umemalizika na wameshaongea naye kila kitu na kabla ya ligi kuanza watampa mkataba mwingine kwani makubaliano katika mkataba wake wa awali ameyafikia na kwamba mkataba unaofuata wataongeza makubaliano mengine ambayo pia Mzambia huyo atatakiwa kuyatimiza katika mkataba mpya.

“Kilichokuwa kinatukwamisha hapo awali ni kocha kuwepo Morogoro, lakini tulichofanikiwa ni kuongea naye na kilichobakia ni kusaini tu mkataba na kabla ya ligi kuanza atakuwa ameshasaini mkataba mpya,” alisema Mkwasa.

Lwandamina alitua Yanga mwaka jana akichukua mikoba ya mholanzi Hans van Plujim ambaye alijiuzulu na  kwa sasa ndiye Kocha mkuu wa matajiri wa mkoani Singida, Klabu ya Singida United.

Mzambia huyo ambaye aliiongoza miamba ya Zambia Zesco United kutinga nusu fainali ya klabu bingwa barani Afrika msimu juzi,alifanikiwa kuiwezesha Yanga kutetea ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa mwaka 2016-17 kwa kuipiku Simba kwa uwiano wa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: