JESHI la polisi mkoani Pwani linamshikilia kijana mmoja mwanaume (17) mkazi wa mbagala Dar es Salaam aliyejifanya mwanamke kwa kuvalia mavazi ya kike kwa lengo linalodaiwa kuwa ni kutaka kufanya uhalifu.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Jonathan Shana alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 3 asubuhi maeneo ya Picha ya Ndege barabara ya kwenda magereza wilaya ya kibaha Mkoa wa Pwani ambapo mtuhumiwa mbali ya kuvaa mavazi ya kike pia alikuwa ameficha uso wake kwa nikabu.
Alisema kijana huyo alikamatwa na polisi akiwa amepandishwa kwenye boda boda baada ya wananchi kutoa taarifa za siri za kumtilia mashaka mtu huyo.
Shana alisema kwa sasa polisi bado wanafanya mahojiano naye ili kujua lengo lake nini na kubaini mtandao wake anaoshirikiana nao katika kufanya uhalifu.
Post A Comment: