ads

MSAJILI wa Vyama vya Siasa ametoa sababu za kukataa tangazo la kufukuzwa uanachama kwa wabunge wawili wa Chama cha Wananchi (CUF) - Magdalena Sakaya na Maftaha Nachuma.


Akizungumza na gazeti la Nipashe jana, Jaji Francis Mutungi alisema taarifa iliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad juu ya kuwavua uanachama wabunge hao haitambui kwa sababu haikuwasilishwa na mtu mwenye dhamana ndani ya chama hicho.

Jaji Mutungi alisema ofisi yake inamtambua Maalim Seif, lakini yeye anaheshimu taarifa ya kukaimu ukatibu mkuu iliyowasilishwa katika ofisi yake na CUF haijatenguliwa na chama hicho.

Jaji Mutungi alisema taarifa iliyowasilishwa na Maalim Seif ya kuwavua uanachama wabunge hao ilipaswa kuwasilishwa na mtu mwenye dhamana ya majukumu ya Katibu Mkuu au Mwenyekiti wa Taifa wa CUF ambao ni Magdalena Sakaya au Profesa Ibrahim Lipumba au wawakilishi wao waliopewa idhini.

Jaji Mutungi alisema kwa mujibu wa katiba ya CUF ibara ya 80 (1) kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Taifa kinaweza kuitishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa au Mwenyekiti wa Chama Taifa ambaye kwa sasa ni Profesa Lipumba.

"Kwa mujibu wa maelezo niliyotoa kuhusu suala la Magdalena Sakaya kukaimu shughuli za Katibu Mkuu basi kwa mantiki hiyo na kwa mujibu wa ibara ya 84(2), Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji Taifa ya chama chenu kwa sasa ni Magdalena Sakaya," alisema Jaji Mutungi.

Aidha, Jaji Mutungi alisema kwa mujibu wa ibara ya 91 (c) vikao vyote vya Baraza Kuu la CUF vinapaswa kuongozwa na Mwenyekiti wa Taifa ambaye ni Profesa Lipumba.

Jaji Mutungi alisema ofisi yake mpaka sasa haijapokea barua yoyote kutoka CUF inayotengua uamuzi wa kumkaimisha ukatibu mkuu, Magdalena Sakaya.

Sakaya ni Mbunge wa jimbo la Kaliua mkoani Tabora na Maftaha ni mbunge wa Mtwara mjini.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: