Mahakama Kuu Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya waliokuwa wabunge wa viti maalum wa Chama cha Wananchi (CUF), waliokuwa wakipinga kuapishwa kwa wabunge wateule.
Wabunge hao walifungua maombi hayo wakiiomba mahakama itoe amri ya zuio kwa Bunge, lisiwaapishe wabunge hao wateule, hadi pale kesi yao ya msingi kupinga kufutwa uanachama wa CUF itakapotolewa hukumu.
Hata hivyo, Mahakama Kuu imeyatupilia mbali maombi hayo, baada ya kukubaliana na hoja za mapingamizi zilizowasilishwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kupitia jopo la mawakili wanane wa Serikali wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata, na wakili wa Bodi ya Wadhamini CUF pamoja na wabunge wateule, Mashaka Ngole.
Malata anawawakilisha Katibu wa Bunge na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Post A Comment: