LEO tunaangalia sifa za nyangumi. Mnyama ambaye ni mkubwa kuliko wote duniani. Kimsingi wanyama hawa wamegawanyika katika aina mbalimbali lakini wote huitwa nyangumi.
Anayezumziwa hapa ni yule anayefahamika kwa jina la kisayansi Balaenoptera musculus ambaye ndiye mkubwa kuliko nyangumi wote na ndiye mnyama ambaye ukubwa wake haujawahi tokea wala kufanana na mnyama mwingine yeyote hata ambao wamekwisha toweka duniani.
SIFA ZAKE
Maziwa ya nyangumi hutawaliwa na kiasi kikubwa cha mafuta kiasi cha kufanya hata ukuaji wa watoto wao kuongezeka haraka.
Anapokamata chakula chake hubeba na kiasi kingi cha maji ambayo huyatoa tena baada ya kuyatenganisha na chakula.
Jike huzaa kila baada ya miaka mitatu.
Nyangumi hupatikana karibia bahari zote duniani.
Jinsia ya kiume ya nyangumi dume huwa na urefu kati ya futi kumi na 12.
Nyangumi dume pamoja kwamba ndiye mwenye maumbile makubwa lakini hayakuumbwa na korodani.
Ingawa mwili wake ni mkubwa kuliko lakini macho yake ni madogo na yenye uwezo mkubwa wa kuona.
Ni mnyama asiyekunywa maji kabisa, hii ni kwa sababu huishi baharini ambako hupatikana maji chumvi ambayo si rafiki kwake, hivyo kiu chake hukatika kwa chakula alichokula ambapo huchakatwa na kufyonzwa majimaji.
Uzito wa moyo wa nyangumi hufanana na uzito wa gari ndogo.
Ulimi wake ukitaka kuubeba basi yakupasa ujihakikishie una uwezo wa kubeba tembo mkubwa.
Ndiye mnyama tajiri kwa hifadhi kubwa ya maziwa.
Kwa asili viumbe hawa huishi kwa mitala, nyangumi dume humiliki majike wengi na hawana matatizo kwakuwa hufahamu madume ni wachache, hivyo jike mmoja anaposhika mimba huwapa nafasi majike wenzie kufurahi na dume wake.
Kama fisi atambulikavyo bwana afya wa msituni, nyangumi hutambuliwa kama miungi wa baharini.
Hana uwezo wa kupumua kwa mdomo kama ilivyo kwa mwanadamu, kwa kuwa mdomo wake huungana na tumbo, hivyo hutumia matundu ya pua tu.
16.Moyo wake umegawanyika katika sehemu nne na mshipa mkuu wa moyo (aorta) ni mkubwa kiasi kwamba mtoto anaweza kuogelea mpaka ndani yake.
Matundu ya mishipa yake ni makubwa mno, binadamu yeyote anaweza kupenya na kutokea upande wa pili.
Kama walivyo wanyama wengine, naye pia huwa na uti wa mgongo.
Ni miongoni mwa viumbe ambao ni urithi wa dunia, hivyo ni mnyama ambaye hawindwi kabisa kama ilivyo kwa wanyama wengine kama tembo.
Kutokana na ukubwa wake awapo baharini hata samaki wakali kama papa huwa hawajaribu kumchokoza kwa kumuhofia, kwa sababu hiyo hubeba sifa ya ubabe baharini.
Mdomoni kwake unaweza kuwapanga binadamu 100 na wakatosha vizuri.
Kwa ukubwa wake, binadamu wameweza kutengeneza hata hadithi ya kwamba anaweza kutengeneza kisiwa na binadamu wakafanya shughuli zao juu ya mgongo wake mpaka hapo atakapoondoka,
ifahamike hadithi hiyo haina ukweli kuhusiana na maisha ya mnyama huyu, ni utunzi wa kufikirika.
Nyangumi ni mnyama mkarimu na mstaarabu wala hawezi kufanya uvamizi kwa binadamu, na hata aonapo vyombo hivyo vya usafiri huvipisha na kwenda kando, hutambua kwamba binadamu hupenda kuwatazama basi agunduapo vyombo hivyo pamoja na kwenda mbali, huanza kufanya mbwembwe ili mumuone ikiwa ni pamoja na kuogelea, kurusha maji na kuurusha mwili wake.
Pamoja kwamba ni mla nyama lakini hali binadamu! Ukiwa kwenye meli akajirusha unaweza kuzimia kwa presha kumbe wala kiumbe wa watu hana hata shida na wewe na anataka ufurahi kumuona.
Kwa hisani ya Mtanzania
Post A Comment: