Ikiwa ni miezi miwili tangu alipoondokewa na mzazi mwenzake, mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zarina Hassan amepata pigo jingine kwa kufiwa na mama yake mzazi, Halima Hassan.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zarina maarufu kwa jina la Zarithebosslady ametangaza kuwa mama yake mzazi aliyekuwa akiugua kwa wiki kadhaa, amefariki duniani katika Hospitali ya Nakasero iliyopo Kampala, nchini Uganda.
Halima alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa zaidi ya wiki moja akisumbuliwa na matatizo ya moyo.
Ameandika kuwa kwa huzuni kubwa pamoja na familia yake anatangaza kifo cha mama yake mpendwa aliyefariki asubuhi ya leo Julai 20.
“Utapendwa milele na wajukuu zake, sisi watoto uliopewa na Mungu tunashukuru kwa yale uliotufanyia, pumzika kwa amani mama,” ameandika Zari.
Kifo cha mama yake kimekuja takribani miezi miwili baada ya Ivan Ssemwanga ambaye ni baba wa watoto watatu wa Zari.
Ssemwanga maarufu Ivan the Don alifariki Mei 25, mwaka huu kutokana na matatizo ya moyo.
Post A Comment: