Salamu za rambirambi zilizotolewa na Profesa Mark Mwandosya kwenye msiba wa mke wa Dk Harrison Mwakyembe jana, ziliibua simanzi kwa waombolezaji kwa jinsi alvyoeleza namna mama huyo alivyomuuguza alipokuwa amelazwa nchini India mwaka 2011.
Mke wa Mwakyembe, Linah alifariki dunia Julai 15 katika Hospitali ya Aga Khan alikokuwa akitibiwa na alizikwa jana wilayani Kyela, Mbeya.
Akitoa salamu za rambirambi katika mazishi hayo, Profesa Mwandosya alimkumbusha Dk Mwakyembe jinsi marehemu alivyowauguza wakiwa India.
Dk Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, aliwahi kutibiwa India kwa wakati mmoja na Profesa Mwandosya.
“Namkumbuka shemeji yangu Linah tulipokuwa tunaumwa India alitufariji sana kwa nyimbo za dini akiwa na mke wangu, hivyo kama kufa tulipaswa kutangulia sisi kwa kuwazidi umri na hata kwa kuumwa. Lakini Mungu amemchukua yeye na sisi tutafuata,” alisema Profesa Mwandosya kauli iliyomfanya Dk Mwakyembe ainamishe kichwa kwa huzuni.
Post A Comment: