Rais John Magufuli amekutana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza mkoani Kagera ambako wanatarajiwa kuwa na mazungumzo.
Nkurunziza amewasili mjini hapa leo Alhamisi, Julai 20 akilakiwa na mwenyeji wake na kupigiwa mizinga 21 ya heshima na kisha kulikagua gwaride maalumu.
Mara baada ya kumaliza ukaguzi wa gwaride hilo viongozi hao wanatarajiwa kuwa na mazungumzo maalumu, ambayo haijafahamika yatakuwa yanahusu jambo gani.
Rais Magufuli yuko ziarani Kanda ya Ziwa na jana alizindua barabara ya kiwango cha lami ya Kagoma- Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa kilomita 154.
Post A Comment: