ads

Matokeo ya kidato cha sita nchini  yametolewa leo Julai 15, na wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo  kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21), huku shule za Mkoa wa Pwani ziking'ara.


Kwa upande wa wavulana,  waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya  46,385. Taarifa iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na wavulana ni 35,647.

“Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la 1-11  umepanda  kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi 93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;


“Pia, ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07 ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana” Taarifa kutoka baraza la mitihani 

Hata hivyo Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.,
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: